Post ya Mgeni. Malezi: Elimu nzuri haiwezi kutatua malezi na misingi mibovu ulioipata utotoni. (Soma Kwa Kiingereza: Read in English)
Tunataka kushiriki sura ya kitabu ilichoandikwa na Agnes, mama ya mwanafunzi na voluntia wa zamani kwetu, Elimu Yetu. Tunatarajia kushirika post za huyu mwandishi mgeni tena.
Malezi
Elimu nzuri haiwezi kutatua malezi na misingi mibovu ulioipata utotoni
Ndugu zangu wasomaji wangu wapendwa. Napenda kuchukua nafasi hili kueleza juu ya malezi ya watoto wetu.
Je mtakubaliana nami kwamba asilimia tisini ya wazazi wamekuwa wakigharamia, elimu nzuri kwa watoto wao kuliko elimu ya maadili. Na malezi ya misingi mizuri kwa watoto. Ninamaanisha elimu ya kuishi na jamii (elimu ya Mtaani). Kwa kudhani kwamba elimu nzuri pekee aliyomrithisha mtoto itasawazisha kila kitu, bila kifikiri au kujali kwamba kuna leo na kesho. Ya kwamba mtoto huyu ni kwa jamii inayomzunguka kama ilivyo desturi kwamba mtoto awapo tumboni ni wako lakini akishazaliwa ni wa jamii.
Ikumbukwe, kwamba elimu nzuri pekee bila malezi mazuri yenye misingi bora bado haujamsaidia mtoto wako, na wala hajakamilika bado. Maana yake hawezi kuishi na jamii inayomzunguka. Kwa nini? Kwanza mtoto huyu hawezi kujitambua, kujikubali, kujiheshimu, hata jamii haiwezi kumkubali kwa sababu mtoto asipokuwa na misingi yenye maadili mazuri matokea yake kijana kama huyu akipata madaraka tunetengemea haya kutoka kwake:
Kiongozi asiyekuwa na adabu
Kiongozi fisadi
Kiongozi asiyekubalika
Kiongozi mbinafsi
Kiongozi asiykuwa na msimamo
Kionogi mwenye upendeleo
Kiongozi katili
Kiongozi bwanyenye
Kiongozi mvivu
Kiongozi asiyekuwa na maaritha ya busara
Kiongozi asiyekuwa na hofu ya mungu
Comments