top of page

Juu ya mitihani: Barua kwa Wazazi [On Exams: A Letter for Parents]


[English below]

Mbona watoto huchukia mitihani mno? Nilipokuwa mtoto, nilijiuliza hili swali mara kwa mara. Mtihani ni kurasa tu, lakini nilikuwa na hofu ya mitihani kuliko Mungu! Siku ya mtihani, nikalia, nikapiga kilele kwa mamangu, “Kwanini lazima niende shuleni? Sitaki! Sina akili! Niokoa mama!” Siku moja, alinisikia na akasema, “Sawa mtoto, Mitihani siyo muhimu. Usiendi, usijali!” na sikuendi. Baadaye nimebadilisha; sasa napenda mithiani kwa kweli!

Mtoto anaposoma kwa ajili ya kufaulu mtihani tu pekee, haina maana. Hata angeyakumbuka masomo yake darasani, angeyasahau barabarani. Mwanafunzi anaposhindwa kufaulu mtihani, usimuadhibu, haswa tafadhali usimchape. Je, ungekubali nami, kama mtoto alitoa juhudi za kutosha, kutofaulu siyo kosa lake? Hili kosa ndilo ni letu; sisi jamii yake, walimu na wazazi. Wangalimfundisha zaidi, angalifanikiwa. Mtihani si kipimo cha mtoto; mtihani ni kipimo cha kazi yetu.

Ukipochapa mtoto kwa sababu ya mtihani ina madhara mabaya kwenye maendeleo yake ya kiakili na kiroho. Bila shuka hatapendi mitihani migumu ya baadaye. Atathamini kazi rahisi kuliko changamoto. Atajifunza kudanganya tu. Kwa pili, huwezi kulazimisha mawazo huru. kusudi la kujifunza huanza moyoni. Mtoto anapoogopa shuleni, anapoteza udadasi, ubunifu, na ujiamini wake.

Nawakumbusha, mtihani siyo umilele. Kujifunza ni mchakato tata na mrefu unaotaka ujitihada. Hiyvo mhimize, na mtia moyo. Baada ya mtihani, usimwambie vitu kama vile “wewe ni mkali” au “wewe ni mjinga.” Hata usisemi “Una akili.” Bora umwambie kwa mfano “Umejifunza vizuri” au “umefanikiwa” au “Umejitihada sana” au “Umeshindwa kuelewa sehemu gani?” Kwa sababu, kuanza na “Wewe ni” inamaana haitabadiliki, lakini kuanza na “ume-“ inamaana inaweza kubadilikwa na juhudi.


Ukiwa na maswali, wasiliana nasi hapa.


[Kwa Kiingereza]


Why do children hate tests so much? When I was a kid, I asked myself this question over and over. A test is just papers, but I had more fear of tests than of God. The day of the test, I’d cry and scream for my mother “Why do I have to school? I don’t want to! I’m not intelligent! Save me mama!” One day she heard me and said, “Ok, kid. Tests aren’t important. Don’t go, don’t worry!”, and I didn’t go. Now I’ve changed, I actually like tests!

When a child studies only in order to pass a test, it has no meaning. Even if he were to remember his lessons in the classroom, he would forget them on the street. When a student fails to pass an exam, do not punish him, especially please do not hit him. Would you agree with me, if a child gave enough effort, not passing is not his fault? This mistake is indeed ours; we his community, teachers and parents. If we had taught him more, he would have succeeded. The exam is not a test of the child; it is a test of our work.

When you hit a child because of an exam, it has bad risks/consequences for his intellectual and spiritual development. Undoubtedly, he will not like hard tests later. He will value easy work over good work. He will only learn to cheat. Secondly, you cannot force free ideas. The intention of learning starts in the heart. When a child is afraid of school, he loses his curiosity, creativity, and self-belief.

I remind you all, an exam is not destiny. Learning is a long and complex process that takes internal struggle. So encourage him, let him take heart. After an exam, don’t tell him things like “You are sharp” or “You are stupid.” Even don’t say “You have intelligence.” It’s better you tell him “You have learned well” or “You have struggled a lot” or ask him “Which part did you fail to understand?” Because, to start with “You are” means that it cannot be changed, but to start with “You have done” means it can be changed with effort.


Please search for your child's exam here, according to his class.

Please contact us with any questions.

Comentários


bottom of page